Master Basic Violin Skills
Kozi hii ya Violin imeandaliwa kwa kutumia kitabu cha Essential Elements 2000 for Strings kama mwongozo mkuu wa mafunzo. Kozi inalenga kumpa mwanafunzi msingi imara wa upigaji wa violin kuanzia hatua ya mwanzo hadi kiwango cha kati (beginner to lower-intermediate), kwa mfumo wa darasa la mtandao wenye maelekezo ya moja kwa moja, mazoezi ya vitendo, na tathmini endelevu kupitia Chemsha Bongo zetu.
Mwisho wa kozi, mwanafunzi ataweza:
Kushika violin na upinde (bow) kwa usahihi (proper posture and bow hold).
Kusoma noti za muziki kwenye staff (Treble Clef).
Kutambua na kupiga noti katika nyuzi zote nne (G, D, A, E strings).
Kutumia fingering sahihi (1–4) kwa usahihi wa sauti.
Kupiga skeli za msingi (kama D Major, A Major, G Major).
Kufuata midundo (rhythm patterns) mbalimbali kwa usahihi.
Kucheza nyimbo rahisi kwa kutumia noti na rhythms alizojifunza.
Kufanya mazoezi kwa kutumia accompaniment tracks (play-along).
Mwanafunzi anahitaji kuwa na vifaa vifuatavyo:
Violin (saizi sahihi kulingana na umri)
Upinde (bow)
Rosin
Shoulder rest
Music stand
Kitabu: Essential Elements 2000 for Strings (waweza kupakua ndani ya platform hii, kimeambatanishwa BURE Kabisa kwa ajili yako)
Tuner (au App ya tuning)
Metronome (au App)
No reviews yet. Be the first to review this course!
Login